Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 12:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku hiyo mtasema:“Nakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu,maana ingawa ulinikasirikia,hasira yako imetulia,nawe umenifariji.

2. Mungu ndiye mwenye kuniokoa,nitamtegemea yeye, wala sitaogopa;Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu;yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.”

3. Mtachota maji kwa furahakutoka visima vya wokovu.

4. Siku hiyo mtasema:“Mshukuruni Mwenyezi-Mungumwombeni kwa jina lake.Yajulisheni mataifa matendo yake,tangazeni kuwa jina lake limetukuka.

5. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifakwa kuwa ametenda mambo makuu;haya na yajulikane duniani kote.

6. Pazeni sauti na kuimba kwa furaha,enyi wakazi wa Siyoni,maana aliye mkuu miongoni mwenundiye Mungu, Mtakatifu wa Israeli.”

Kusoma sura kamili Isaya 12