Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 11:3-12 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.

4. Atawapatia haki watu maskini,atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.Kwa neno lake ataiadhibu dunia,kwa tamko lake atawaua waovu.

5. Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.

6. Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.Ndama na wanasimba watakula pamoja,na mtoto mdogo atawaongoza.

7. Ngombe na dubu watakula pamoja,ndama wao watapumzika pamoja;na simba atakula majani kama ng'ombe.

8. Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyokamtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.

9. Katika mlima mtakatifu wa Munguhakutakuwa na madhara wala uharibifu.Maana kumjua Mwenyezi-Mungu kutaenea pote nchini,kama vile maji yajaavyo baharini.

10. Siku ile chipukizi wa Yese atakuwa ishara kwa mataifa; mataifa yatamtafuta na makazi yake yatatukuka.

11. Siku hiyo, Bwana ataunyosha mkono wake tena kuwarejesha watu wake waliosalia huko Ashuru, Misri, Pathrosi, Kushi, Elamu, Shinari, Hamathi na sehemu za pwani.

12. Naye atatweka bendera kuwaashiria mataifa,kuwakusanya Waisraeli waliodharauliwa,kuwaleta pamoja watu wa Yuda waliotawanywa,na kuwarudisha toka pembe nne za dunia.

Kusoma sura kamili Isaya 11