Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 11:13-16 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Wivu wa Efraimu juu ya Yuda utakoma,hakutakuwa tena na uadui kati ya Yuda na Efraimu.

14. Wote pamoja watawavamia Wafilisti walio magharibi,pamoja watawapora watu wakaao mashariki.Watawashinda Waedomu na Wamoabu,nao Waamoni watawatii.

15. Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu,kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate,nao utagawanyika katika vijito saba,watu wavuke humo miguu mikavu.

16. Tena, kutakuwa na barabara kuu toka Ashurukwa ajili ya watu wake waliobaki humokama ilivyokuwa kwa Waisraeliwakati walipotoka nchini Misri.

Kusoma sura kamili Isaya 11