Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 10:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ole wao wanaotunga sheria zisizo za haki,watu wanaopitisha sheria za kukandamiza.

2. Huwanyima maskini haki zao,na kuwaibia maskini wa watu wangu maslahi yao.Wajane wamekuwa nyara kwao;yatima wamekuwa mawindo yao.

3. Je, mtafanya nini siku ya adhabu,siku dhoruba itakapowajieni kutoka mbali?Mtamkimbilia nani kuomba msaada?Mtakwenda wapi kuweka mali yenu?

4. Litakalowabakia ni kujikunyata kati ya wafungwana kuangamia pamoja na wanaouawa vitani.Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.

5. Ole wake Ashuru, fimbo ya hasira yangu,yeye ashikaye kiboko cha hasira yangu!

6. Nilimtuma kuliadhibu taifa ovu,nilimwamuru kuwaadhibu watu niliowakasirikia,kuwapora na kuteka nyara,na kuwakanyaga chini kama tope njiani.

7. Lakini Ashuru hakudhamiria hivyo,yeye alikuwa na nia nyingine;alikusudia kuharibu kabisa,kuangamiza mataifa mengi iwezekanavyo.

8. Maana alisema:“Je, si kweli majemadari wangu ni wafalme?

9. Je, si kweli kwamba Kalno nitautenda kama Karkemishi,mji wa Hamathi kama mji wa Arpadi,Samaria kama Damasko?

10. Kama nimefaulu kuunyosha mkono wangudhidi ya falme zenye sanamu za miungukubwa kuliko sanamu za Yerusalemu na Samaria;

11. je, nitashindwa kuutenda Yerusalemu na sanamu zake,kama nilivyoutenda Samaria na sanamu zake?”

Kusoma sura kamili Isaya 10