Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 8:11-14 Biblia Habari Njema (BHN)

11. “Watu wa Efraimu wamejijengea madhabahu nyingi,na madhabahu hizo zimewazidishia dhambi.

12. Hata kama ningewaandikia sheria zangu mara nyingi,wao wangeziona kuwa kitu cha kigeni tu.

13. Wanapenda kutoa tambiko,na kula nyama yake;lakini mimi Mwenyezi-Mungu sipendezwi hata kidogo.Mimi nayakumbuka makosa yao;nitawaadhibu kwa dhambi zao;nitawarudisha utumwani Misri.

14. Waisraeli wamemsahau Muumba wao,wakajijengea majumba ya fahari;watu wa Yuda wamejiongezea miji ya ngome,lakini mimi nitaipelekea moto miji hiyo,na kuziteketeza ngome zao.”

Kusoma sura kamili Hosea 8