Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 8:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Pigeni baragumu!Adui anakuja kama taikuivamia nyumba ya Mwenyezi-Mungu,kwa kuwa wamelivunja agano languna kuiasi sheria yangu.

2. Waisraeli hunililia wakisema:‘Mungu wetu, sisi tunakujua.’

3. Lakini Israeli amepuuza mambo mema,kwa hiyo, sasa adui watamfuatia.

4. “Walijiwekea wafalme bila kibali changu,walijiteulia viongozi ambao sikuwatambua.Wamejitengenezea miungu ya fedha na dhahabu,jambo ambalo litawaangamiza.

5. Watu wa Samaria, naichukia sanamu yenu ya ndama.Hasira yangu inawaka dhidi yenu.Mtaendelea mpaka lini kuwa na hatia?

6. Nanyi Waisraeli ni hivyohivyo!Na sanamu yenu hiyo fundi ndiye aliyeitengeneza.Yenyewe si Mungu hata kidogo.Naam! Sanamu ya ndama ya Samaria itavunjwavunjwa!

7. “Wanapanda upepo, watavuna kimbunga!Mimea yao ya nafaka iliyo mashambanihaitatoa nafaka yoyote.Na hata kama ikizaa,mazao yake yataliwa na wageni.

8. Waisraeli wamemezwa;sasa wamo kati ya mataifa mengine,kama chombo kisicho na faida yoyote;

Kusoma sura kamili Hosea 8