Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 6:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Maana ninachotaka kwenu ni upendo na si tambiko,Kumjua Mungu na si kutoa sadaka za kuteketezwa.

7. “Lakini mlilivunja agano langukama mlivyofanya mjini Adamu;huko walinikosea uaminifu.

8. Gileadi ni mji wa waovu,umetapakaa damu.

9. Kama wanyang'anyi wamwoteavyo mtu njiani,ndivyo na makuhani walivyojikusanya na kuvizia.Wanaua watu njiani kuelekea Shekemu,naam, wanatenda uovu kupindukia.

10. Nimeona jambo la kuchukiza sanamiongoni mwa Waisraeli:Watu wa Efraimu wanakimbilia miungu minginenaam, Waisraeli wamejitia unajisi.

11. Nawe Yuda hali kadhalika,nimekupangia wakati utakapovuna adhabu.

Kusoma sura kamili Hosea 6