Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 23:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Balaamu akamtolea Balaki kauli yake, akasema,“Balaki amenileta hapa kutoka Aramu,naam, mfalme wa Moabu amenileta kutoka milima ya mashariki.‘Njoo uwalaani watu wa Yakobo kwa ajili yangu,naam, njoo uwalaumu Waisraeli!’

8. Nitamlaanije mtu ambaye Mungu hakumlaani?Nitawalaumuje watu ambao Mwenyezi-Mungu hakuwalaumu?

9. Kutoka vilele vya majabali nawaona;kutoka juu ya milima nawachungulia.Hilo taifa likaalo peke yake,lisilojiona kuwa sawa na mataifa mengine.

10. Nani awezaye kuwahesabu wingi wa watu wa Yakobo,au kukisia umati wa Waisraeli?Nife kifo cha waadilifu,mwisho wangu na uwe kama wao.”

11. Hapo, Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nimekuleta hapa uwalaani adui zangu, lakini badala yake umewabariki!”

12. Balaamu akamwambia Balaki, “Sina budi kusema maneno aliyonipa Mwenyezi-Mungu.”

Kusoma sura kamili Hesabu 23