Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 23:15-22 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Balaamu akamwambia Balaki, “Baki hapa karibu na sadaka yako ya kuteketezwa, nami niende kule ngambo kukutana na Mwenyezi-Mungu.”

16. Mwenyezi-Mungu akakutana na Balaamu, akampa maneno atakayosema, na kumwambia arudi kwa Balaki.

17. Basi, Balaamu akarudi, akamkuta Balaki amesimama karibu na sadaka ya kuteketezwa pamoja na maofisa wote wa Moabu. Balaki akamwuliza, “Mwenyezi-Mungu amekuambia nini?”

18. Hapo, Balaamu akamtolea Balaki kauli yake:“Inuka, Balaki, usikie,nisikilize ewe mwana wa Sipori.

19. Mungu si mtu, aseme uongo,wala si binadamu, abadili nia yake!Je, ataahidi kitu na asikifanye,au kusema kitu asikitimize?

20. Tazama, nimepewa amri ya kubariki,naye amebariki wala siwezi kuitangua.

21. Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo,wala udhia kwa hao wana wa Israeli.Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao,Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao,yeye huzipokea sifa zao za kifalme.

22. Mungu aliyewachukua kutoka Misri,huwapigania kwa nguvu kama za nyati.

Kusoma sura kamili Hesabu 23