Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 16:43-50 Biblia Habari Njema (BHN)

43. Mose na Aroni walikwenda, wakasimama mbele ya hema la mkutano,

44. na Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose,

45. “Jitenge na watu hawa, niwaangamize mara moja!”Lakini wao wakajitupa chini kifudifudi.

46. Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako, kitie moto na kukiweka kando ya madhabahu, kisha ukitie ubani halafu uende nacho haraka kwa watu na kuwafanyia upatanisho. Fanya haraka! Ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imekwisha wafikia na pigo limeanza kuwashambulia.”

47. Basi, Aroni akafanya kama alivyoambiwa na Mose. Alichukua chetezo chake na kukimbia hadi katikati ya watu waliokuwa wamekusanyika pamoja. Alipoona kwamba pigo limekwisha anza, alitia ubani katika chetezo na kuwafanyia watu upatanisho.

48. Alipofanya hivyo, pigo hilo lilikoma, naye akabaki katikati ya waliokufa na walio hai.

49. Idadi ya watu waliokufa kwa pigo ilikuwa 14,700, bila kuhesabu wale waliokufa kutokana na uasi wa Kora.

50. Pigo lilipokoma, Aroni alirudi kwa Mose mlangoni mwa hema la mkutano.

Kusoma sura kamili Hesabu 16