Agano la Kale

Agano Jipya

Hagai 1:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku ya kwanza ya mwezi wa sita mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario wa Persia, Mwenyezi-Mungu alimpa Hagai ujumbe aupeleke kwa Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mkuu wa Yuda, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki.

2. Hagai akasema: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Watu hawa wanasema kwamba wakati wa kulijenga upya hekalu langu haujafika.”

3. Lakini Mwenyezi-Mungu ameniambia mimi nabii Hagai,

4. “Je, ni sawa kwenu kukaa katika majumba yenu ya fahari hali hekalu langu ni magofu matupu?”

5. Sasa, asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Fikirini kama mnafanya sawa!

6. Nyinyi mmepanda mbegu kwa wingi, lakini mmevuna kidogo; mnakula, lakini hamshibi; mnakunywa divai, lakini hamtosheki; mnavaa nguo, lakini bado mnasikia baridi; mfanyakazi mshahara wake huwa kama umetumbukizwa katika mfuko uliotoboka.”

7. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Fikirini kama mnafanya sawa!

Kusoma sura kamili Hagai 1