Agano la Kale

Agano Jipya

Habakuki 3:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Sala ya nabii Habakuki:

2. Ee Mwenyezi-Mungu, nimesikia juu ya fahari yako,juu ya matendo yako, nami naogopa.Uyafanye tena mambo hayo wakati wetu;uyafanye yajulikane wakati huu wetu.Ukasirikapo tafadhali ukumbuke huruma yako!

3. Mungu amekuja kutoka Temani,Mungu mtakatifu kutoka mlima Parani.Utukufu wake umetanda pote mbinguni,nayo dunia imejaa sifa zake.

4. Mng'ao wake ni kama wa jua;miali imetoka mkononi mwakeambamo nguvu yake yadhihirishwa.

5. Maradhi yanatangulia mbele yake,nyuma yake yanafuata maafa.

6. Akisimama dunia hutikisika;akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka.Milima ya milele inavunjwavunjwa,vilima vya kudumu vinadidimia;humo zimo njia zake za kale na kale.

7. Niliwaona watu wa Kushani wakiteseka,na watu wa Midiani wakitetemeka.

8. Ee Mwenyezi-Mungu, je, umeikasirikia mito?Je, umeyakasirikia maji ya bahari,hata ukaendesha farasi wako,na magari ya vita kupata ushindi?

9. Uliuweka tayari uta wako,ukaweka mishale yako kwenye kamba.Uliipasua ardhi kwa mito.

10. Milima ilikuona, ikanyauka;mafuriko ya maji yakapita humo.Vilindi vya bahari vilinguruma,na kurusha juu mawimbi yake.

11. Jua na mwezi vilikaa kimya katika makazi yao,vilipoona miali ya mishale yako ikienda kasi,naam, vilipouona mkuki wako ukimetameta.

12. Kwa ghadhabu ulipita juu ya nchi,uliyakanyaga mataifa kwa hasira yako.

Kusoma sura kamili Habakuki 3