19. Hao waliahidi kuwaacha wake zao, na wakatoa kondoo dume kuwa sadaka kwa ajili ya hatia yao.
20. Ukoo wa Imeri: Hanani na Zebadia.
21. Ukoo wa Harimu: Maaseya, Elia, Shemaya, Yehieli na Uzia.
22. Ukoo wa Pashuri: Eliehoenai, Maaseya, Ishmaeli, Nethaneli, Yozabadi na Elasa.
23. Walawi: Yozabadi, Shimei, Kelaya (aliyejulikana pia kama Kelita), Pethahia, Yuda na Eliezeri.