Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 48:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kuanzia mpaka wa kaskazini kwenye barabara ya Hethloni hadi kuingia Hamathi hadi mji wa Hazar-enoni (ulioko mpakani mwa Damasko na Hamathi upande wa kaskazini na kuendelea kutoka mashariki hadi magharibi), eneo hilo litakuwa la kabila la Dani.

2. Eneo linalopakana na la Dani, kutoka mashariki hadi magharibi litakuwa la Asheri.

3. Kabila la Naftali, litapata eneo linalopakana na lile la Asheri, kutoka mashariki hadi magharibi.

4. Baada ya eneo la kabila la Naftali, litafuata eneo la kabila la Manase, kutoka mashariki hadi magharibi.

5. Eneo linalopakana na eneo la Manase, kutoka upande wa mashariki hadi magharibi, litakuwa la kabila la Efraimu.

6. Eneo linalopakana na eneo la Efraimu, kutoka mashariki hadi magharibi, litakuwa la kabila la Reubeni.

7. Eneo linalopakana na eneo la Reubeni, kutoka mashariki hadi magharibi litakuwa la kabila la Yuda.

8. Baada ya eneo la kabila la Yuda, utatenga eneo lenye urefu wa kilomita 12 na upana kama huohuo, kutoka kaskazini hadi kusini, na urefu huohuo kutoka mashariki hadi magharibi, sawasawa na eneo la kabila lolote. Hapo katikati ya eneo hilo patakuwa na maskani ya Mungu.

9. Eneo utakalotenga kwa ajili ya Mwenyezi-Mungu litakuwa lenye urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kwa kilomita 10.

10. Makuhani watakuwa na eneo lao katika eneo hilo. Eneo hilo litakuwa na urefu wa kilomita kumi na mbili u nusu kutoka mashariki hadi magharibi, na kilomita 5 kutoka kaskazini hadi kusini. Maskani ya Mungu itakuwa katikati ya eneo hilo.

11. Eneo hilo litakuwa kwa ajili ya makuhani wa wazawa wa Sadoki, ambao walinitumikia kwa uaminifu na hawakuasi wakati Waisraeli walipoasi kama Walawi walivyofanya.

12. Hilo litakuwa eneo lao maalumu kutoka katika eneo takatifu la nchi, eneo takatifu kabisa, litakalopakana na eneo la Walawi.

Kusoma sura kamili Ezekieli 48