Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 35:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Wewe mtu! Ugeukie mlima Seiri, utoe unabii juu ya wakazi wake.

3. Uambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Mimi napambana nawe, ee mlima Seiri. Ninanyosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya uwe jangwa na ukiwa.

4. Ninaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa jangwa. Ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

5. Ulikuwa adui wa daima wa Israeli, ukasababisha watu wake wauawe kwa upanga, wakati wa msiba wao, wakati wa adhabu yao ya mwisho.

6. Kwa hiyo, kama niishivyo, nasema mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, naapa kwamba kifo kinakungoja na hutaweza kukikwepa. Kwa kuwa unayo hatia ya mauaji, basi mauaji nayo yatakuandama.

7. Nitaufanya mlima Seiri kuwa ukiwa na jangwa na yeyote apitaye huko nitamwangamiza.

8. Nitajaza milima yako watu waliouawa; na katika vilima vyako na mabonde yako na magenge yako yote watakuwako waliouawa kwa upanga.

9. Nitakufanya kuwa jangwa milele, na miji yako haitakaliwa tena. Ndipo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

10. “Wewe ulisema ya kwamba mataifa hayo mawili yaani Yuda na Israeli ni mali yako na kwamba utazimiliki! Ulisema hivyo ingawa humo ni makao yangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Ezekieli 35