Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 33:31-33 Biblia Habari Njema (BHN)

31. Basi, hukujia makundi kwa makundi na kuketi mbele yako kama watu wangu, wasikie unachosema, lakini hawafanyi unachowaambia wafanye. Wanasema kwamba wana upendo, lakini hayo ni maneno matupu; wanachotafuta kwa moyo ni faida yao tu.

32. Kwao, wewe umekuwa tu kama mwimbaji wa kutumbuiza mwenye sauti nzuri ikiandamana na muziki safi! Wanayasikia yale unayosema, lakini hawatekelezi hata mojawapo.

33. Lakini hayo unayosema yatakapotukia – nayo kweli yatatukia – basi, ndipo watakapotambua kuwa nabii amekuwapo miongoni mwao.”

Kusoma sura kamili Ezekieli 33