Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 33:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Wewe mtu! Ongea na wananchi wenzako, uwaambie hivi: Kama nikizusha vita katika nchi fulani, na watu wa nchi hiyo wakamchagua mmoja wao awe mlinzi wao,

3. huyo anapoona maadui wanakuja, atapiga tarumbeta na kuwaonya watu.

4. Mtu akisikia sauti ya tarumbeta lakini akapuuza onyo hilo, maadui wakaja na kumuua, yeye mwenyewe atawajibika kwa kifo chake.

5. Aliisikia sauti ya tarumbeta, akapuuza onyo; basi lawama ya kifo chake itakuwa juu yake mwenyewe. Lakini kama angejali hilo onyo, angeyaokoa maisha yake.

6. “Lakini kama yule mlinzi akiona adui wanakuja asipige tarumbeta na watu wakawa hawakuonywa juu ya hatari inayokuja, maadui wakaja na kumuua mtu yeyote miongoni mwao; huyo mtu aliyekufa, atakuwa amekufa kwa kosa lake. Lakini mimi nitamdai mlinzi kifo cha mtu huyo.

7. “Basi, ewe mtu, nimekuweka kuwa mlinzi wa Waisraeli. Utakaposikia neno kutoka kwangu utawapa onyo langu.

Kusoma sura kamili Ezekieli 33