Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 28:20-24 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

21. “Wewe mtu! Ugeukie mji wa Sidoni,

22. utoe unabii juu yake kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi:Mimi nitapambana nawe Sidoni,na kuudhihirisha utukufu wangu kati yako.Nitakapotekeleza hukumu zangu juu yakona kukudhihirishia utakatifu wangu,ndipo utakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.

23. Nitakupelekea maradhi mabayana umwagaji damu utafanyika katika barabara zako.Utashambuliwa kwa upanga toka pande zotena watu wako watakaouawa, watakuwa wengi.Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu.”

24. Mungu asema, “Mataifa jirani na Waisraeli ambayo yalikuwa yanawaudhi hayataweza tena kuwaumiza Waisraeli kama vile kwa miiba na michongoma. Ndipo watakapojua ya kuwa mimi ni Bwana Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Ezekieli 28