Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 27:1-18 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Sasa ewe mtu, imba utenzi huu wa maombolezo juu ya mji wa Tiro,

3. mji ule kando ya bahari, unaofanya biashara na mataifa ya pwani. Uambie: Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi:Ewe Tiro, wewe umejigambau mzuri kwelikweli!

4. Mipaka yako imeenea kwelikweli!Umejengwa kama meli nzuri.

5. Wajenzi wako walitumia misonobari kutoka Senirikupasua mbao zako zote;walichukua mierezi kutoka Lebanonikukutengenezea mlingoti.

6. Walichukua mialoni toka Bashaniwakakuchongea makasia yako;walikitengenezea silahakwa misonobari ya kisiwa cha Kupro,na kuipamba kwa pembe.

7. Kitani kilichotariziwa kutoka Misrikilikuwa kwa kupamba tanga lakona kwa ajili ya bendera yako.Chandarua chako kilitengenezwakwa rangi ya samawati na urujuanikutoka visiwa vya Elisha.

8. Watu wa Sidoni na Arvadiwalikuwa wapiga makasia wako.Wenye hekima wako walikuwa ndaniwakifanya kazi kama wanamaji.

9. Wazee wa Gebali na mafundi waowalikuwa kwako kuziba nyufa zako.Mabaharia waliokuwa wakipitia kwakowalifanya biashara nawe.

10. Watu kutoka Persia, Ludi na Putiwalijiunga katika jeshi lako;walirundika kwenye kambi zao za jeshingao zao na kofia zao.Wanajeshi hao walikupatia fahari.

11. Watu wa Arvadi na wa Hele na jeshi lao walilinda kuta zako pande zote, nao watu wa Gamadi walilinda minara yako. Walitundika ngao zao kwenye kuta zako pande zote, na hivyo wakaukamilisha uzuri wako.

12. Watu wa Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mwingi na wa kila namna. Walitoa fedha, chuma, bati, na risasi kupata bidhaa zako.

13. Watu wa Yavani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, wakakupatia watumwa na vifaa vya shaba wapate bidhaa zako.

14. Bidhaa zako uliziuza huko Beth-togarma ili kujipatia farasi wa mizigo na wa vita, ngamia na nyumbu.

15. Watu wa Dedani walifanya biashara nawe. Nchi nyingi za pwani zilikuwa masoko yako maalumu. Watu wake walikuletea pembe za ndovu na mipingo kulipia bidhaa zako.

16. Watu wa Edomu walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa bidhaa zako. Kwa kupata bidhaa zako walikupa akiki, vitambaa vya urujuani, vitambaa vilivyonakshiwa, kitani safi, matumbawe na yakuti.

17. Hata watu wa Yuda na Israeli walifanya biashara nawe; walikupa ngano, zeituni, tini za mwanzoni, asali, mafuta na marhamu kulipia bidhaa zako.

18. Watu wa Damasko walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa bidhaa zako; walikupa divai kutoka Helboni na sufu nyeupe.

Kusoma sura kamili Ezekieli 27