Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21
  22. 22
  23. 23
  24. 24
  25. 25
  26. 26
  27. 27
  28. 28
  29. 29
  30. 30
  31. 31
  32. 32
  33. 33
  34. 34
  35. 35
  36. 36
  37. 37
  38. 38
  39. 39
  40. 40
  41. 41
  42. 42
  43. 43
  44. 44
  45. 45
  46. 46
  47. 47
  48. 48

Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 27 Biblia Habari Njema (BHN)

Maombolezo juu ya Tiro

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia:

2. “Sasa ewe mtu, imba utenzi huu wa maombolezo juu ya mji wa Tiro,

3. mji ule kando ya bahari, unaofanya biashara na mataifa ya pwani. Uambie: Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi:Ewe Tiro, wewe umejigambau mzuri kwelikweli!

4. Mipaka yako imeenea kwelikweli!Umejengwa kama meli nzuri.

5. Wajenzi wako walitumia misonobari kutoka Senirikupasua mbao zako zote;walichukua mierezi kutoka Lebanonikukutengenezea mlingoti.

6. Walichukua mialoni toka Bashaniwakakuchongea makasia yako;walikitengenezea silahakwa misonobari ya kisiwa cha Kupro,na kuipamba kwa pembe.

7. Kitani kilichotariziwa kutoka Misrikilikuwa kwa kupamba tanga lakona kwa ajili ya bendera yako.Chandarua chako kilitengenezwakwa rangi ya samawati na urujuanikutoka visiwa vya Elisha.

8. Watu wa Sidoni na Arvadiwalikuwa wapiga makasia wako.Wenye hekima wako walikuwa ndaniwakifanya kazi kama wanamaji.

9. Wazee wa Gebali na mafundi waowalikuwa kwako kuziba nyufa zako.Mabaharia waliokuwa wakipitia kwakowalifanya biashara nawe.

10. Watu kutoka Persia, Ludi na Putiwalijiunga katika jeshi lako;walirundika kwenye kambi zao za jeshingao zao na kofia zao.Wanajeshi hao walikupatia fahari.

11. Watu wa Arvadi na wa Hele na jeshi lao walilinda kuta zako pande zote, nao watu wa Gamadi walilinda minara yako. Walitundika ngao zao kwenye kuta zako pande zote, na hivyo wakaukamilisha uzuri wako.

12. Watu wa Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mwingi na wa kila namna. Walitoa fedha, chuma, bati, na risasi kupata bidhaa zako.

13. Watu wa Yavani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, wakakupatia watumwa na vifaa vya shaba wapate bidhaa zako.

14. Bidhaa zako uliziuza huko Beth-togarma ili kujipatia farasi wa mizigo na wa vita, ngamia na nyumbu.

15. Watu wa Dedani walifanya biashara nawe. Nchi nyingi za pwani zilikuwa masoko yako maalumu. Watu wake walikuletea pembe za ndovu na mipingo kulipia bidhaa zako.

16. Watu wa Edomu walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa bidhaa zako. Kwa kupata bidhaa zako walikupa akiki, vitambaa vya urujuani, vitambaa vilivyonakshiwa, kitani safi, matumbawe na yakuti.

17. Hata watu wa Yuda na Israeli walifanya biashara nawe; walikupa ngano, zeituni, tini za mwanzoni, asali, mafuta na marhamu kulipia bidhaa zako.

18. Watu wa Damasko walifanya biashara nawe kwa sababu ya wingi wa bidhaa zako; walikupa divai kutoka Helboni na sufu nyeupe.

19. Vedani na Yavani walisafirisha bidhaa zako toka Uzali; hata chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai ili kupata bidhaa zako.

20. Watu wa Dedani walifanya biashara nawe kwa kukupatia matandiko ya farasi.

21. Waarabu na wakuu wote wa nchi ya Kedari walikuwa wachuuzi wako wakuu katika biashara ya wanakondoo, kondoo madume na mbuzi.

22. Wachuuzi wa Sheba na wa Rama walifanya biashara nawe; walikuletea viungo vya chakula, vito vya thamani na dhahabu kujipatia bidhaa zako safi.

23. Wakazi wa miji ya Harani, Kane na Edeni na wachuuzi wa Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe.

24. Hao walifanya nawe biashara ya mavazi ya fahari, nguo za buluu zilizotariziwa, mazulia ya rangi angavu vifundo na kamba zilizosokotwa imara.

25. Merikebu za Tarshishi ndizo zilikusafirishia bidhaa zako.Basi kama meli katikati ya bahariwewe ulikuwa umejaa shehena.

26. Wapiga makasia wako walikupeleka mbali baharini.Upepo wa mashariki umekuvunjavunjaukiwa mbali katikati ya bahari.

27. Utajiri wako wa bidhaa na mali,wanamaji wako wote chomboni,mafundi wako wa meli na wachuuzi wako,askari wako wote walioko kwako,pamoja na wasafiri walioko kwako,wote wataangamia baharini,siku ile ya kuangamizwa kwako.

28. Mlio wa mabaharia wako utakaposikika,nchi za pwani zitatetemeka.

29. Hapo wapiga makasia wotewataziacha meli zao.Wanamaji na manahodha watakaa pwani.

30. Wataomboleza kwa uchungu wa moyo juu yako,na kulia kwa uchungu mkubwa;watajitupia mavumbi vichwani mwaona kugaagaa kwenye majivu.

31. Wamejinyoa vichwa kwa ajili yakona kuvaa mavazi ya gunia.Watalia kwa uchungu wa moyo juu yako.

32. Wataimba wimbo wa ombolezo juu yako;‘Nani aliyepata kuangamizwa kama Tirokatikati ya bahari?’

33. Bidhaa zako zilipowasili nchi za ngambo,ulitosheleza mahitaji ya watu wengi!Kwa wingi wa utajiri wa bidhaa zakouliwatajirisha wafalme wa dunia.

34. Lakini sasa umevunjikia baharini;umeangamia katika vilindi vya maji.Shehena yako na jamii ya mabahariavimezama pamoja nawe.

35. Wakazi wote wa visiwaniwamepigwa na bumbuazi juu yako;wafalme wao wameogopa kupindukia,nyuso zimekunjamana kwa huzuni.

36. Wachuuzi wa mataifa watakufyonya!Umeufikia mwisho wa kutisha,na hutakuwapo tena milele!”