Agano la Kale

Agano Jipya

Ezekieli 17:15-19 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Lakini yule mfalme mpya alimwasi mfalme wa Babuloni kwa kuwatuma wajumbe Misri kuomba farasi na askari wengi. Je, mfalme huyo atafaulu? Je, anayefanya hivyo na kuvunja agano lake ataweza kuepa adhabu?

16. “Mimi Mwenyezi-Mungu naapa kwamba, kama niishivyo, mfalme huyu atafia katika nchi ya Babuloni, nchi ya mfalme yule aliyemweka awe mfalme, na ambaye amedharau kile kiapo na kuvunja lile agano alilofanya naye.

17. Hakika, Farao pamoja na jeshi lake kubwa hataweza kumsaidia vitani wakati Wababuloni watakapomzungushia ngome na kuta ili kuwaua watu wengi.

18. Kwa kuwa alikidharau kile kiapo na kuvunja lile agano ambalo aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na kufanya mambo haya yote, hakika hataokoka.

19. “Kwa hiyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema, kama niishivyo, kwa vile amekidharau kiapo alichoapa kwa jina langu na agano langu akalivunja, hakika nitamwadhibu vikali.

Kusoma sura kamili Ezekieli 17