Agano la Kale

Agano Jipya

Danieli 6:18-28 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Kisha mfalme akarudi katika ikuluni yake ambamo alikesha akifunga; hakufanya tafrija ya aina yoyote, na usingizi ukampaa.

19. Alfajiri na mapema, mfalme Dario aliamka, akaenda kwa haraka kwenye pango la simba.

20. Alipofika karibu akamwita Danieli kwa sauti ya huzuni, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai! Je, Mungu wako unayemtumikia daima ameweza kukuokoa na simba hawa?”

21. Danieli akamjibu mfalme, “Uishi, ee mfalme!

22. Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.”

23. Hapo mfalme akafurahi sana; akaamuru Danieli atolewe pangoni. Basi wakamtoa, naye alikuwa hajadhurika hata kidogo, kwa sababu alimtegemea Mungu wake.

24. Mfalme akaamuru wale watu waliomchongea Danieli wakamatwe, nao wakatupwa ndani ya lile pango la simba pamoja na wake zao na watoto wao. Nao, hata kabla hawajagusa chini, simba waliwashambulia na kuivunjavunja mifupa yao.

25. Ndipo mfalme Dario akawaandikia watu wa makabila yote, mataifa yote, na lugha zote duniani:“Nawatakieni amani kwa wingi.

26. Nitatoa amri kwamba watu wote katika ufalme wangu ni lazima wamwogope na kumcha Mungu wa Danieli.“Yeye ni Mungu aliye hai, aishiye milele;ufalme wake kamwe hauwezi kuangamizwa,utawala wake hauna mwisho.

27. Yeye hukomboa na kuokoa,hufanya ishara na maajabu mbinguni na duniani,maana amemwokoa Danieli makuchani mwa simba.”

28. Basi, Danieli akapata fanaka wakati wa utawala wa mfalme Dario na wa mfalme Koreshi, Mpersi.

Kusoma sura kamili Danieli 6