Agano la Kale

Agano Jipya

Amosi 6:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ole wenu nyinyi mnaostarehe huko Siyoni,nanyi mnaojiona salama mlimani Samaria!Nyinyi mwaonekana kuwa viongozi wa taifa maarufuambao Waisraeli wote huwategemea.

2. Haya! Nendeni Kalne mkaangalie kila mahali,tokeni huko mwende hadi mji ule mkubwa wa Hamathi,kisha teremkeni hadi Gathi kwa Wafilisti.Je, falme zao si bora kuliko zenuna eneo lao si bora kuliko lenu?”

3. Nyinyi mnajaribu kuifukuza siku mbaya.Lakini mnauleta karibu utawala dhalimu.

4. Ole wenu mnaolala juu ya vitanda vya pembe za ndovuna kujinyosha juu ya masofa,mkila nyama za wanakondoo na ndama!

5. Nyinyi mnapenda kuimba ovyo na sauti ya vinubina kubuni ala mpya za muziki mkimwiga mfalme Daudi.

6. Mnakunywa divai kwa mabakuli,na kujipaka marashi mazuri mno.Lakini hamhuzuniki hata kidogojuu ya kuangamia kwa wazawa wa Yosefu.

7. Kwa hiyo mtakuwa wa kwanza kwenda uhamishoni,na karamu za wenye kustarehe zitatoweka.

8. Bwana Mwenyezi-Mungu ameapa kwa nafsi yake;Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi asema:“Nachukizwa mno na kiburi cha wazawa wa Yakobo;tena nayachukia majumba yao ya fahari.Mji wao na vyote vilivyomo nitawapa adui zao.”

9. Kama wakibaki watu kumi katika nyumba moja, wote watakufa.

Kusoma sura kamili Amosi 6