Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 21:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Nayo sanamu ya Ashera aliyotengeneza akaiweka katika nyumba ambayo Mwenyezi-Mungu aliizungumzia mbele ya Daudi na mwanawe Solomoni: “Katika nyumba hii na mjini Yerusalemu niliouchagua ndiko mahali nitakapoabudiwa milele.

8. Na iwapo Waisraeli watajali kutenda yote niliyowaamuru na kufuata Sheria zote mtumishi wangu Mose alizowapa, basi sitawaacha wafukuzwe kutoka katika nchi hii ambayo niliwapa babu zao.”

9. Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.

10. Ndipo Mwenyezi-Mungu alisema kupitia kwa watumishi wake manabii,

11. “Kwa sababu mfalme amefanya mambo ya kuchukiza, mambo mabaya zaidi ya yale yaliyotendwa na Waamori waliomtangulia, amewafanya watu wa Yuda pia watende dhambi kwa kutumia sanamu zake;

12. basi, sasa, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, tazama nitaleta juu ya Yerusalemu na Yuda, msiba ambao hata yeyote atakayesikia atashtuka.

13. Nitauadhibu Yerusalemu kama vile nilivyofanya Samaria, na mfalme Ahabu na wazawa wake. Nitafuta Yerusalemu kama mtu afutavyo sahani iliyosafishwa na kuiinamisha.

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 21