Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 21:17-26 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Matendo mengine ya Manase na yote aliyotenda, pamoja na dhambi zake zote, yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Yuda.

18. Manase alifariki na kuzikwa katika bustani ya nyumba yake mwenyewe, katika Bustani ya Uza. Naye Amoni mwanawe akatawala mahali pake.

19. Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili huko Yerusalemu. Jina la mama yake ni Meshulemethi, binti Haruzi wa Yothba.

20. Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, kama vile Manase baba yake alivyofanya.

21. Alifuata njia yote aliyoiendea baba yake na kutumikia sanamu ambazo baba yake alizitumikia na kuziabudu.

22. Alimwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zake, hakushika njia ya Mwenyezi-Mungu.

23. Baadaye watumishi wa Amoni walikula njama na kumwua katika ikulu yake.

24. Lakini watu wa Yuda wakawaua wote waliomuua Amoni. Kisha watu hao wa Yuda wakamtawaza Yosia mwanawe mahali pake.

25. Matendo mengine yote ya Amoni yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda.

26. Amoni alizikwa kaburini katika bustani ya Uza; na Yosia mwanawe akatawala mahali pake.

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 21