Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 21:10-17 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Ndipo Mwenyezi-Mungu alisema kupitia kwa watumishi wake manabii,

11. “Kwa sababu mfalme amefanya mambo ya kuchukiza, mambo mabaya zaidi ya yale yaliyotendwa na Waamori waliomtangulia, amewafanya watu wa Yuda pia watende dhambi kwa kutumia sanamu zake;

12. basi, sasa, mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, tazama nitaleta juu ya Yerusalemu na Yuda, msiba ambao hata yeyote atakayesikia atashtuka.

13. Nitauadhibu Yerusalemu kama vile nilivyofanya Samaria, na mfalme Ahabu na wazawa wake. Nitafuta Yerusalemu kama mtu afutavyo sahani iliyosafishwa na kuiinamisha.

14. Nitawaacha hao watu wa urithi wangu watakaosalia na kuwakabidhi kwa adui zao; watakuwa mawindo na mateka kwa adui zao wote.

15. Nitawatendea hayo yote kwa sababu wameniasi na kunikasirisha tangu wazee wao walipotoka Misri mpaka leo.”

16. Zaidi ya hayo, licha ya dhambi yake alipowakosesha watu wa Yuda wakafanya dhambi kwa kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Manase aliwaua watu wengi wasiokuwa na hatia, damu ilijaa toka upande mmoja mpaka upande mwingine wa Yerusalemu.

17. Matendo mengine ya Manase na yote aliyotenda, pamoja na dhambi zake zote, yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Yuda.

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 21