Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 19:17-28 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Ee Mwenyezi-Mungu, ni kweli kwamba wafalme wa Ashuru wameangamiza mataifa na nchi zao.

18. Walitupa miungu yao motoni kwa sababu haikuwa miungu ya kweli, bali sanamu za miti na mawe zilizochongwa na mikono ya watu.

19. Sasa, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, nakusihi utuokoe makuchani mwa Senakeribu, falme zote za dunia zijue kwamba ni wewe peke yako, ee Mwenyezi-Mungu, uliye Mungu.”

20. Kisha Isaya, mwana wa Amozi akatuma ujumbe kwa Hezekia, akisema, “Hivi ndivyo anavyosema Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ‘Nimesikia ombi lako kwangu kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru:’

21. Hili ndilo neno la Mwenyezi-Mungu alilosema kumhusu Senakeribu:Anakudharau, anakubeza binti Siyoni,anatikisa kichwa chake nyuma yako binti Yerusalemu.

22. Je, uliyekuwa unamkashifu na kumdhihaki ni nani?Nani umemwinulia sautina kumkodolea macho kwa kiburi?Juu ya Mtakatifu wa Israeli!”

23. Kwa kuwatuma wajumbe wako umemkashifu Bwana,wewe umesema, “Kwa magari yangu mengi ya vita,nimekwea vilele vya milimampaka kilele cha Lebanoni.Nimekata mierezi yake mirefu,na misonobari mizurimizuri;nimeingia mpaka ndani yakena ndani ya misitu yake mikubwa.

24. Nimechimba visimana kunywa maji mageninilikausha mito yote ya Misrikwa nyayo za miguu yangu.

25. ‘Je, hujasikia,kwamba nilipanga jambo hili tangu awali?Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani.’Nilikuweka uijenge miji yenye ngomekwa rundo la magofu.

26. Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu,wametishika na kufadhaika,wamekuwa kama mimea ya shambani,kama majani yasiyo na nguvu.Kama majani yaotayo juu ya paa;yakaukavyo kabla ya kukua.

27. Najua kuketi kwako,na kuamka kwakonako kuingia kwako;nayo mipango yako dhidi yangu.

28. Kwa vile umefanya mipango dhidi yanguna nimeusikia ufidhuli wako,nitatia ndoana yangu puani mwako,na lijamu yangu kinywani mwako.Nitakurudisha njia ileile uliyojia.”

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 19