Agano la Kale

Agano Jipya

2 Wafalme 15:34-38 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Kama vile Uzia baba yake, Yothamu alitenda mambo yaliyompendeza Mwenyezi-Mungu.

35. Hata hivyo, mahali pa kuabudia miungu ya uongo hapakuharibiwa, na watu waliendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani kwenye mahali pa juu. Yothamu alijenga lango la kaskazini la nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

36. Matendo mengine ya Yothamu na yote aliyofanya yameandikwa katika Kitabu cha Mambo ya Nyakati za Wafalme wa Yuda.

37. Wakati wa enzi ya Yothamu, Mwenyezi-Mungu alianza kutuma mfalme Resini wa Aramu na mfalme Peka wa Israeli ili kushambulia Yuda.

38. Yothamu akafariki na kuzikwa katika makaburi ya kifalme katika mji wa Daudi. Mwanae Ahazi alitawala mahali pake.

Kusoma sura kamili 2 Wafalme 15