Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 22:44-51 Biblia Habari Njema (BHN)

44. “Wewe uliniokoa na mashambulizi ya watu wangu,umenifanya mtawala wa mataifa.Watu nisiowajua walinitumikia.

45. Wageni walinijia wakinyenyekea,mara waliposikia habari zangu walinitii.

46. Wageni walikufa moyo;wakaja kutoka ngome zao wakitetemeka.

47. “Mwenyezi-Mungu yu hai!Asifiwe mwamba wangu!Atukuzwe Mungu wangu, mwamba wa wokovu wangu.

48. Yeye ameniwezesha kulipiza kisasina kuyatiisha mataifa chini yangu.

49. Ameniokoa kutoka adui zangu.Ee Mwenyezi-Mungu, ulinikuza juu ya wapinzani wanguna kunisalimisha mbali na watu wakatili.

50. “Kwa hiyo, nitakutukuza kati ya mataifa,ee Mwenyezi-Mungu, nitaliimbia sifa jina lako.

51. Mungu humjalia mfalme wake ushindi mkubwa;humwonesha fadhili zake huyo aliyemweka wakfu,naam, humfadhili Daudi na wazawa wake milele.”

Kusoma sura kamili 2 Samueli 22