Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 22:33-41 Biblia Habari Njema (BHN)

33. Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara,na ameifanya njia yangu iwe salama.

34. Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa,na kuniweka salama juu ya vilele.

35. Hunifunza kupigana vita,mikono yangu iweze kuvuta upinde wa shaba.

36. Umenipa ngao yako ya kuniokoa;msaada wako umenifanya mkuu.

37. Umenirahisishia njia yangu;wala miguu yangu haikuteleza.

38. Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza,sikurudi nyuma mpaka wameangamizwa.

39. Niliwaangamiza, nikawaangusha chiniwasiweze kuinuka tena;walianguka chini ya miguu yangu.

40. Wewe ulinijalia nguvu ya kupigana vita;uliwaporomosha adui chini yangu.

41. Uliwafanya adui zangu wakimbie,na wale walionichukia niliwaangamiza.

Kusoma sura kamili 2 Samueli 22