Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 22:2-17 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Alisema,“Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu,ngome yangu, na mkombozi wangu.

3. Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama;ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu,ngome yangu na kimbilio langu.Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili.

4. Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie,nami naokolewa kutoka kwa adui zangu.

5. “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira,mafuriko ya maangamizi yalinivamia;

6. kamba za kuzimu zilinizinga,mitego ya kifo ilinikabili.

7. “Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu;nilimwita Mungu wangu.Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu,kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

8. “Hapo, dunia ikatetemeka na kutikisika,misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka,kwani Mungu alikuwa amekasirika.

9. Moshi ulifuka kutoka puani mwake,moto uunguzao ukatoka kinywani mwake,makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.

10. Aliinamisha anga, akashuka chini;na wingu jeusi chini ya miguu yake.

11. Alipanda kiumbe chenye mabawa na kuruka,alionekana juu ya mabawa ya upepo.

12. Alijizungushia giza pande zote,kifuniko chake kilikuwa mawingu mazito na mkusanyiko wa maji.

13. Umeme ulimulika mbele yake,kulilipuka makaa ya moto.

14. Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni,Mungu Mkuu akatoa sauti yake.

15. Aliwalenga adui mishale, akawatawanya,alirusha umeme, akawatimua.

16. Mwenyezi-Mungu alipowakemea,kutokana na pumzi ya puani mwake,vilindi vya bahari vilifunuliwa,misingi ya dunia ikaonekana.

17. “Mungu alinyosha mkono wake toka juu, akanichukua,kutoka kwenye maji mengi alininyanyua.

Kusoma sura kamili 2 Samueli 22