18. Aliniokoa kutoka kwa adui yangu mwenye nguvu,aliniokoa kutoka kwa hao walionichukiamaana walikuwa na nguvu nyingi kunishinda.
19. Walinivamia nilipokuwa taabuni,lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu.
20. Alinileta, akaniweka mahali pa usalama,alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.
21. “Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu;alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia.
22. Maana, nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu,wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu.
23. Nimeshika maagizo yake yote,sikuacha kufuata masharti yake.
24. Mbele yake sikuwa na hatia,nimejikinga nisiwe na hatia.
25. Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu,yeye anajua usafi wangu.