Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 22:15-22 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Aliwalenga adui mishale, akawatawanya,alirusha umeme, akawatimua.

16. Mwenyezi-Mungu alipowakemea,kutokana na pumzi ya puani mwake,vilindi vya bahari vilifunuliwa,misingi ya dunia ikaonekana.

17. “Mungu alinyosha mkono wake toka juu, akanichukua,kutoka kwenye maji mengi alininyanyua.

18. Aliniokoa kutoka kwa adui yangu mwenye nguvu,aliniokoa kutoka kwa hao walionichukiamaana walikuwa na nguvu nyingi kunishinda.

19. Walinivamia nilipokuwa taabuni,lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu.

20. Alinileta, akaniweka mahali pa usalama,alinisalimisha, kwani alipendezwa nami.

21. “Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu;alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia.

22. Maana, nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu,wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu.

Kusoma sura kamili 2 Samueli 22