Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 22:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Daudi alimwimbia Mwenyezi-Mungu maneno ya wimbo ufuatao siku ile Mwenyezi-Mungu alipomkomboa mikononi mwa adui zake, na mkononi mwa Shauli.

2. Alisema,“Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu,ngome yangu, na mkombozi wangu.

3. Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama;ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu,ngome yangu na kimbilio langu.Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili.

4. Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie,nami naokolewa kutoka kwa adui zangu.

5. “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira,mafuriko ya maangamizi yalinivamia;

6. kamba za kuzimu zilinizinga,mitego ya kifo ilinikabili.

7. “Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu;nilimwita Mungu wangu.Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu,kilio changu kilimfikia masikioni mwake.

8. “Hapo, dunia ikatetemeka na kutikisika,misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka,kwani Mungu alikuwa amekasirika.

Kusoma sura kamili 2 Samueli 22