Agano la Kale

Agano Jipya

2 Samueli 1:15-20 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Kisha, Daudi akamwita mmoja wa vijana wake akamwambia, “Muue mtu huyu!” Yule kijana alimpiga yule Mmaleki, naye akafa.

16. Daudi akasema, “Uwajibike wewe mwenyewe kwa kifo chako, maana umejishuhudia wewe mwenyewe kwa mdomo wako ukisema, ‘Nimemuua mtu aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu kwa kupakwa mafuta.’”

17. Daudi aliimba ombolezo lifuatalo kwa ajili ya Shauli na mwanawe Yonathani.

18. Daudi alisema watu wa Yuda wafundishwe ombolezo hilo, nalo limeandikwa katika kitabu cha Yashari. Daudi aliimba,

19. “Walio fahari yako, ee Israeli,wameuawa milimani pako.Jinsi gani mashujaa walivyoanguka!

20. Jambo hilo msiuambie mji wa Gathiwala katika mitaa ya Ashkeloni.La sivyo, wanawake Wafilisti watashangilia,binti za wasiotahiriwa, watafurahi.

Kusoma sura kamili 2 Samueli 1