Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 7:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Solomoni alipomaliza sala yake, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuchoma sadaka na tambiko za kuteketeza zilizotolewa, kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukaijaza nyumba.

2. Kwa kuwa utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa nyumba ya Mwenyezi-Mungu, makuhani hawakuweza kuingia humo.

3. Waisraeli wote walipoona moto ukishuka kutoka mbinguni na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulijaa katika nyumba walisujudu nyuso zao zikifika mpaka sakafuni, wakamwabudu na kumshukuru Mwenyezi-Mungu wakisema,“Kwa kuwa ni mwema,fadhili zake zadumu milele.”

4. Kisha mfalme Solomoni na watu wote walimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko.

5. Naye Solomoni alimtolea Bwana ng'ombe 22,000 na kondoo 120,000. Hivyo ndivyo Solomoni na watu wote walivyoiweka wakfu nyumba ya Mungu.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 7