Agano la Kale

Agano Jipya

2 Mambo Ya Nyakati 26:20-23 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Azaria, kuhani mkuu, na wale makuhani wengine, walimtazama, kisha wakaharakisha kumtoa nje; hata yeye mwenyewe akafanya haraka kutoka, kwa maana Mwenyezi-Mungu alikuwa amemwadhibu.

21. Basi, mfalme Uzia akawa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Alikaa katika nyumba yake ya pekee kwani hakukubaliwa tena kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Naye Yothamu mtoto wake, akatunza jamaa yake huku akitawala wakazi wa nchi.

22. Matendo mengine yote ya mfalme Uzia kutoka mwanzo mpaka mwisho, yaliandikwa na nabii Isaya mwana wa Amozi.

23. Uzia alifariki na kuzikwa katika eneo la kuzikia wafalme, kwa sababu walisema, “Yeye ana ukoma”. Naye Yothamu mwanawe, akatawala mahali pake.

Kusoma sura kamili 2 Mambo Ya Nyakati 26