Agano la Kale

Agano Jipya

1 Wafalme 18:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ikawa baada ya siku nyingi, mnamo mwaka wa tatu wa ukame, neno hili la Mwenyezi-Mungu likamjia Elia: “Nenda ukajioneshe kwa mfalme Ahabu, halafu nitanyesha mvua nchini.”

2. Basi, Elia akaenda kujionesha kwa Ahabu.Wakati huo, njaa ilikuwa kali sana huko Samaria.

3. Basi, Ahabu akamwita Obadia msimamizi wa ikulu. (Obadia alikuwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu sana,

4. na wakati Yezebeli alipowaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, Obadia aliwachukua manabii 100, akawaficha hamsinihamsini pangoni, akawa anawapelekea chakula na maji).

Kusoma sura kamili 1 Wafalme 18