Agano la Kale

Agano Jipya

1 Samueli 2:5-14 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele,sasa wanaajiriwa ili wapate chakula.Lakini waliokuwa na njaa,sasa hawana njaa tena.Mwanamke tasa amejifungua watoto saba.Lakini mama mwenye watoto wengi,sasa ameachwa bila mtoto.

6. Mwenyezi-Mungu huua na hufufua;yeye huwashusha chini kuzimunaye huwarudisha tena.

7. Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini,na baadhi wawe matajiri.Wengine huwashusha,na wengine huwakweza.

8. Huwainua maskini toka mavumbini;huwanyanyua wahitaji toka majivuni,akawaketisha pamoja na wakuu,na kuwarithisha viti vya heshima.Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu;yeye ameisimika dunia juu ya minara yake.

9. “Maisha ya waaminifu wake huyalinda,lakini maisha ya waovu huyakatilia mbali gizani.Maana, binadamu hapati ushindi kwa nguvu zake.

10. Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande;atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni.Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote;atampa nguvu mfalme wakeataukuza uwezo wa mteule wake.”

11. Kisha, Elkana akarudi nyumbani Rama. Lakini mtoto Samueli akabaki Shilo kumtumikia Mwenyezi-Mungu chini ya uongozi wa kuhani Eli.

12. Watoto wa kiume wa Eli walikuwa walaghai sana. Hawakumjali Mwenyezi-Mungu

13. wala juu ya vitu ambavyo watu walipaswa kuwapa makuhani. Kila mara mtu alipokuwa anatolea tambiko yake, mtumishi wa kuhani alikuja na uma wenye meno matatu; na wakati nyama ikiwa bado inachemka,

14. huyo mtumishi aliuchomeka uma huo ndani ya chungu, nyama yoyote iliyotolewa humo na uma huo, ilikuwa mali ya kuhani. Waisraeli wote waliokwenda Shilo kutolea tambiko zao walitendewa hivyo.

Kusoma sura kamili 1 Samueli 2