Agano la Kale

Agano Jipya

1 Samueli 14:25-27 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Watu wote walipofika sehemu yenye msitu, walikuta asali kila mahali.

26. Ingawa watu walipofika msituni na kukuta asali ikidondoka kila mahali hakuna mtu aliyethubutu kula asali hiyo kwa kuogopa kile kiapo walichoapishwa.

27. Lakini Yonathani hakuwa amesikia baba yake alipowaapisha watu. Hivyo akainyosha fimbo aliyokuwa nayo, akaichovya kwenye sega la asali, akala asali hiyo. Hapo akajisikia kuwa na nguvu.

Kusoma sura kamili 1 Samueli 14