Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 9:7-23 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Na wa wazawa wa Benyamini: Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;

8. na Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu, mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya;

9. na ndugu zao, sawasawa na vizazi vyao; watu956. Watu hao wote ndio waliokuwa wakuu wa koo za baba zao, kwa kadiri ya koo za baba zao.

10. Makuhani wafuatao waliishi Yerusalemu: Yedaya, Yehoyaribu na Yakini,

11. na Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu, mkuu wa nyumba ya Mungu;

12. na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri;

13. wakuu wa koo za baba zao; pamoja na ndugu zao; jumla watu 1,760. Walikuwa wakuu wenye uwezo mkubwa katika huduma yote ya nyumba ya Mungu.

14. Walawi wafuatao waliishi Yerusalemu: Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari;

15. na Bakbakari, na Hereshi, na Galali, Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu;

16. na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokuwa wakiishi katika vijiji vya Wanetofathi.

17. Walinzi wa hekalu wafuatao pia waliishi katika Yerusalemu: Shalumu, Akubu, Talmoni na Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mkuu wao.

18. Hadi kufikia wakati huo, walinzi kutoka katika koo zao ndio waliolinda Lango la mfalme la upande wa mashariki. Hapo awali, walikuwa walinzi wa maingilio ya makambi ya Walawi.

19. Shalumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, pamoja na ndugu zake wa ukoo wa Kora, walikuwa na wajibu wa kuyatunza maingilio ya hema la mkutano, kama vile walivyokuwa babu zake wakati wa ulinzi wa kambi ya Mwenyezi-Mungu.

20. Finehasi, mwana wa Eleazari, alikuwa msimamizi wao, hapo awali, naye Mwenyezi-Mungu alikuwa pamoja naye.

21. Zekaria mwana wa Meshelemia, pia alikuwa mlinzi wa maingilio ya hema la mkutano.

22. Jumla, watu 212 walichaguliwa kuwa walinzi wa maingilio ya hekalu. Waliandikishwa kulingana na vijiji walimoishi. Mfalme Daudi na Samueli mwonaji ndio waliowathibitisha katika wadhifa huu muhimu.

23. Basi, watu hao na wazawa wao, waliendelea kuyalinda malango ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 9