Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 8:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Benyamini alikuwa na wana watano: Bela, mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli wa pili, Ahara wa tatu,

2. Noha wa nne na Rafa wa tano.

3. Bela naye alikuwa na wana: Adari, Gera, Abihudi,

4. Abishua, Naamani, Ahoa,

5. Gera, Shufamu na Huramu.

6. Hawa ndio wazawa wa Ehudi. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa za wale waliokuwa wakiishi Geba, lakini wakachukuliwa mateka uhamishoni Manahathi;

7. Naamani, Ahiya na Gera. Gera, baba yake Uza na Ahihudi, ndiye aliyewaongoza kuchukua hatua hiyo.

8. Shaharaimu aliwapa talaka wake zake wawili, Hushimu na Baara na baadaye alipata watoto wa kiume nchini Moabu.

9. Alimwoa Hodeshi, naye akamzalia wana saba: Yoabu, Sibia, Mesha, Malkamu,

10. Yeuzi, Sakia, na Mirma. Hawa wanawe wote walikuja kuwa wakuu wa koo.

11. Shaharaimu na mkewe Hushimu alipata wana wengine wawili: Abitubu na Elpaali.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 8