Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 7:29-40 Biblia Habari Njema (BHN)

29. Na pia mipakani mwa wana wa Manase: Beth-sheani na vitongoji vyake, Taanaki na vitongoji vyake, Megido na vitongoji vyake na Dori na vitongoji vyake. Hiyo ndiyo miji walimoishi wazawa wa Yosefu, mwana wa Israeli.

30. Hawa ndio wazawa wa Asheri. Asheri alikuwa na wana wanne: Imna, Ishva, Ishri na Beria, na binti mmoja jina lake Sera.

31. Beria alikuwa na wana wawili: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

32. Heberi alikuwa na wana watatu: Yafleti, Shomeri na Hothamu, na binti mmoja jina lake Shua.

33. Yafleti pia alikuwa na wana watatu: Pasaki, Bimhali na Ashvathi.

34. Shemeri, nduguye, alikuwa na wana watatu: Roga, Yehuba na Aramu.

35. Na Helemu, ndugu yake mwingine, alikuwa na wana wanne: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

36. Wana wa Sofa walikuwa Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,

37. Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera.

38. Wana wa Yetheri walikuwa Yefune, Pispa na Ara.

39. Wana wa Ula walikuwa Ara, Hanieli na Risia.

40. Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 7