Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 27:16-26 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Hii ndiyo orodha ya wakuu wa makabila ya Israeli: Wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; Eliezeri ndiye aliyekuwa ofisa mkuu; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka;

17. wa Lawi, Hashabia mwana wa Kemueli; wa Aroni, Sadoki;

18. wa Yuda, Elihu, mmoja wa ndugu za mfalme Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;

19. wa Zebuluni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeremothi mwana wa Azrieli;

20. wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia; wa nusu ya kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;

21. wa nusu ya kabila la Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; na wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;

22. wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Israeli.

23. Mfalme Daudi hakuwahesabu wale waliokuwa chini ya umri wa miaka ishirini kwa maana Mwenyezi-Mungu aliahidi kuwaongeza Waisraeli wawe wengi kama nyota za mbinguni.

24. Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu lakini hakumaliza; tena ghadhabu iliwapata Waisraeli kwa ajili ya tendo hili, nayo hesabu hiyo haikuingizwa katika kumbukumbu za mfalme Daudi.

25. Aliyesimamia hazina za mfalme Daudi alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli. Yonathani mwana wa Uzia alisimamia hazina zilizokuwa mashambani, mijini, vijijini na ngomeni.

26. Aliyewasimamia wakulima alikuwa Ezri mwana wa Kelubu.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 27