Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 14:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha mfalme Hiramu wa Tiro alituma wajumbe kwa Daudi, pia alimpelekea mierezi, waashi na maseremala, ili wamjengee Daudi ikulu.

2. Hivyo, Daudi akatambua kwamba Mwenyezi-Mungu amemwimarisha awe mfalme wa Israeli, na kwamba ufalme wake umekuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.

3. Huko Yerusalemu, Daudi alioa wake wengi zaidi, naye akazaa wana na mabinti wengine.

4. Yafuatayo ndio majina ya watoto aliozaa huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni,

5. Ibhari, Elishua, Elpeleti,

6. Noga, Nefegi, Yafia,

7. Elishama, Beeliada na Elifeleti.

8. Wafilisti waliposikia kwamba Daudi amepakwa mafuta kuwa mfalme wa nchi nzima ya Israeli, wote walitoka kwa wingi kwenda kumtafuta. Daudi alipopata habari, alitoka kwenda kuwakabili.

9. Wafilisti walifika wakaanza mashambulizi katika bonde la Refaimu.

10. Ndipo Daudi alipomwuliza Mungu shauri, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Naye Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”

11. Basi, Daudi akaenda huko Baal-perasimu, akawashinda; halafu akasema, “Mungu amepita katikati ya adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo panaitwa Baal-perasimu.

12. Wafilisti walipokimbia, waliziacha sanamu za miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri zote zichomwe moto.

13. Kisha Wafilisti walifanya mashambulizi katika bonde hilo kwa mara ya pili.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 14