Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 1:9-23 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.

10. Kushi alimzaa Nimrodi, aliyekuwa mtu shujaa wa kwanza duniani.

11. Wazawa wa Misri ni Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi,

12. Wapathrusi Wakaftori na Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti).

13. Wana wa Kanaani walikuwa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi.

14. Kanaani pia ndiye babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

15. Wahivi, Waarki, Wasini,

16. Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

17. Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuri, Arpaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

18. Arpaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi.

19. Eberi alikuwa na wana wawili; mmoja wao aliitwa Pelegi, (kwa maana wakati wake watu walikuwa wametawanyika duniani), na ndugu yake aliitwa Yoktani.

20. Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

21. Hadoramu, Uzali, Dikla,

22. Obali, Abimaeli, Sheba,

23. Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 1