Agano la Kale

Agano Jipya

1 Mambo Ya Nyakati 1:38-47 Biblia Habari Njema (BHN)

38. Wana wa Seiri walikuwa Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.

39. Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.

40. Wana wa Shobali walikuwa Alvani, Manahathi, Ebali, Shefi na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa Aya na Ana.

41. Mwana wa Ana alikuwa Dishoni; na wana wa Dishoni walikuwa Hamrani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

42. Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani na Akani; na wana wa Dishoni walikuwa Usi na Arani.

43. Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.

44. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake.

45. Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemi alitawala badala yake.

46. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu.

47. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka alitawala badala yake.

Kusoma sura kamili 1 Mambo Ya Nyakati 1