Agano la Kale

Agano Jipya

Yakobo 3:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja?

12. Ndugu zangu, je, mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.

13. Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.

14. Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.

15. Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.

16. Maana popote palipo na wivu na ubinafsi, hapo pana fujo na kila aina ya uovu.

17. Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.

18. Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani.

Kusoma sura kamili Yakobo 3