Agano la Kale

Agano Jipya

Waroma 12:7-15 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe.

8. Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.

9. Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema.

10. Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

11. Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana.

12. Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima.

13. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu.

14. Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani.

15. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia.

Kusoma sura kamili Waroma 12