Agano la Kale

Agano Jipya

Wakolosai 1:8-19 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Yeye alitupa habari za upendo wenu mliojaliwa na Roho.

9. Kwa sababu hiyo tumekuwa tukiwaombeeni daima tangu wakati tulipopata habari zenu. Tunamwomba Mungu awajazeni ujuzi kamili wa matakwa yake, pamoja na hekima yote na ujuzi wa kiroho.

10. Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.

11. Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili muweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.

12. Na kwa furaha mshukuruni Baba, aliyewawezesha nyinyi kuwa na sehemu yenu katika mambo yale aliyowawekea watu wake katika ufalme wa mwanga.

13. Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi.

14. Kwake yeye tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa.

15. Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana;ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.

16. Maana kwake vitu vyote viliumbwakila kitu duniani na mbinguni,vitu vinavyoonekana na visivyoonekana:Wenye enzi, watawala, wakuu na wenye nguvu.Vyote viliumbwa kwake na kwa ajili yake.

17. Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote;vyote huendelea kuwako kwa uwezo wake.

18. Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa;yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili.Yeye ndiye mwanzo,mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka kwa wafu,ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.

19. Maana Mungu alipenda utimilifu wake wote uwe ndani yake.

Kusoma sura kamili Wakolosai 1